Twalib awakashifu wanaokosoa mshikamano wa Raila na Rais Uhuru

May 12, 2018

BADI TWALIB

Mbunge wa Jomvu Badi Twalib amekashifu hatua ya baadhi ya viongozi wanaokashifu mshikamano wa Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga  akisema kuwa lengo lao ni kuvuruga uhusiano huo.

Kulingana na Badi mshikamano wa viongozi hao wawili ulilenga kuliunganisha taifa na tayari umeleta muafaka humu nchini.

Mbunge huyo aidha amewataka viongozi kote nchini kujitenga na siasa za kuwagawanya wananchi na badala yake washirikiane kikamili kuliendeleza taifa.

 Wakati uo huo amewataka viongozi kuzipa nafasi kamati zilizoundwa ili kuona kwamba zinaafikia malengo yake.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.