Uchunguzi waanzishwa kuhusu mkasa wa moto katika hoteli ya Leopard

February 11, 2019

Idara ya usalama kaunti ya Kwale imeanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na mkasa wa moto uliotokea katika hoteli ya kifahari ya Leopard kule Diani kaunti ya Kwale usiku wa kuamkia leo.

Kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amesema waliokuwa ndani ya hoteli hiyo ikiwemo Wazari wa Ugatuzi Eugine Wamalwa ni kati ya waliokolewa na hakuna mtu yeyote aliyejerihiwa wakati wa mkasa huo.

Amesema tayari usalama umeimarishwa ndani na nje ya hoteli hiyo, akisema polisi watatoa taarifa kamili baada ya kukamilisha uchunguzi wao kuhusiana na mkasa huo.

Hata hivyo walioshuhudia mkasa huo, wamesema moto huo ulisababishwa na milipoko ya Fataki zilizokuwa zikirushwa na wageni waliokuwa wakisheherekea sherehe zao katika hoteli hiyo mwendo wa saa nne usiku hapo jana.

Usimamizi wa hoteli hiyo ya kifahari ya Leopard bado haujazunguzia kuhusu mkasa huo licha ya wanahabari wetu kujitahizi kupata taarifa kutoka kwao.

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.