Ugavi wa ardhi kwa wakaazi 665 waanza Mombasa

May 29, 2018

Mgogoro wa ardhi unaoikumba ardhi iliyo ya ukubwa wa ekari 39 huko Junda eneo bunge la Kisauni kaunti ya Mombasa sasa unaelekea kikomo baada ya Mbunge wa eneo hilo Ali Mbogo kuzindua mpango wa kuipima na kuigawa ardhi hiyo kwa Wakaazi.

Mbogo na Naibu Rais William Ruto wametoa kima cha shilingi milioni moja kuanzisha mipangilio hiyo mara moja na kuhakikisha kila mkaazi anapimiwa ardhi yake na kuishi bila ya hofu ya kufurushwa.

Akizungumza huko Junda alipoanzisha mpango wa kuigawa ardhi hiyo kwa jumla ya Wakaazi 665 Mbogo amewataka Wakaazi kuwa wavumilivu akisema katika kipindi cha miezi minne ijayo swala hilo litakuwa limepata suluhu ya kudumu.

Mbunge huyo wa Kisauni amefichua kwamba juma lijalo mikakati sawa na hiyo itaanzishwa katika ardhi inayokabiliwa na mzozo ya Majaoni ili kutatua migogoro hiyo ya ardhi mara moja.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.