Uhaba wa maji kushuhudiwa baada ya bomba kupasuka mzima

September 5, 2018

BOMBA 2

Wakaazi wa kaunti ya Taita taveta watasalia bila maji safi kwa muda baada ya bomba la kusambaza maji  kutoka Chemichemi ya maji ya Mzima kupasuka.

Waziri wa Maji katika serikali ya kaunti hiyo Gasper Kabaka amesema shughuli za kukarabati wa bomba hilo la kusambaza maji zimeanza, huku akiwataka wananchi kuwa na subra.

Amesema hali ya kawaida ya sambazaji maji itarejea punde tu ukarabati huo utakapokamilika kwani serikali ya kaunti hiyo inafaa vyema kuwa wananchi wanapitia changamoto hiyo.

Hata hivyo wananchi wa kaunti hiyo wameilaumu pakubwa kampuni ya kusambaza maji katika kaunti hiyo kufuatia muundo msingi duni huku wakidai kuwa swala hilo limewasababishia changamoto kubwa.

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.