Uhasama waibuka kati ya Gavana Mvurya na Mbunge wa Kinango

May 14, 2018

Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amemshtumu vikali Mbunge wa Kinango Benjamin Dalu Tayari, kwa kuendeleza siasa za ukabila na mgawanyiko.

Akiongea huko Mazeras  eneo bunge la Kinango,   Mvurya amesema kwamba  Tayari  na baadhi ya wawakilishi wa Wadi wanaolenga nyadhifa kuu mwaka wa 2022, wamekuwa wakiwagawanya  wakaazi  wa Kinango kwa  msingi wa kikabila.

MVURYA 14 05 18 (1)

Gavana huyo aidha amewapuuza viongozi wanaokosoa uongozi wake, akisema kwamba wakaazi wa Kwale wamenufaika na miradi mingi ya maendeleo kupitia kwa uongozi wake.

Hata hivyo mbunge wa Kinango Benjamin Tayari amejibu kauli za Gavana Mvurya akimtaka kutoingilia siasa za uchaguzi mkuu ujao, kwa kuwalazimisha wakaazi wa Kwale kwa viongozi wasiowataka.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.