Ukosefu wa vifaa wapelekea wanafunzi 157 kukosa kufanya mtihani wa Kemia

November 9, 2018

Hali ya Sintofahamu imetanda katika shule ya upili ya Brightways huko Malindi hii ni baada ya Jumla ya wanafunzi 157  kukosa kufanya mtihani wa “practical”  wa Kemia kufuatia ukosefu wa vifaa vya somo hilo katika maabara ya shule hiyo.

Wanafunzi hao wamelazimika kuhamishiwa shule ya upili ya Barani ili kutafuta namna ya kukalia mtihani huo baada ya kukwama shuleni mwao kwa zaidi ya saa sita.

Ni hali ambayo imezua  wasi wasi miongoni mwa maafisa wasimamizi wa mtihani huo na kupelekea polisi  kuingilia kati na kuwatia nguvuni wakurugenzi wawili wa shule hiyo kwa majina Ibrahim Komora pamoja na Oscar Mirembe, ambao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Malindi waakiendelea kuchunguzwa.

Hata hivyo juhudi za kuzungumza na mkuu wa elimu kaunti ndogo ya Malindi Veronicah Kalungu hazikufua dafu baada yake kukataa katakata kuzungumza na wanahabari.

Taarifa kutoka kwa polisi  zimefichua kuwa shule hiyo haikuwa na umeme, Gesi, sambamba na kemikali za kufanyia mtihani huo.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.