Ukosefu wa vyoo wazua hofu Garashi

July 9, 2018

Bodi ya shule ya upili ya Garashi huko Magarini kaunti ya Kilifi imeitaka serikali kuingilia kati kukabili uhaba wa vyoo vya wanafunzi unaoshuhudiwa katika shule hiyo.

Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Samson Thoya amesema kuwa wanafunzi wa kike katika shule hiyo wanapitia hali ngumu zaidi kutokana na uhaba wa vyoo shuleni humo.

Thoya amesema kuwa wanahofia kwamba ukosefu wa vyoo vya kutosha katika unahatarisha afya ya wananfunzi, huku akiitaka serikali kupitia wizara ya afya kuingilia kati kuikabili hali hiyo.

Akigusia suala la uhaba wa waalimu Thoya amesema kuwa kwa sasa shule hiyo inawaalimu wacheche ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi na kusisitiza kuajiriwa waalimu zaidi ilikuboresha viwango vya elimu.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.