Upakaji wa rangi Mombasa waungwa mkono na washikadau

July 7, 2018

Washikadau katika sekta ya utalii kaunti ya Mombasa wamepongeza hatua ya serikali ya kaunti hiyo ya kushurutisha wamiliki wa majumba katikati ya mji huo kupaka rangi majumba yao.

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa mkurugenzi wa chama cha watalii kanda ya pwani Julius Owino amesema kuwa hatua hio ya kurembesha mji itasaidia pakuwa kuinua viwango vya utalii katika kaunti hio.

Owino vile vile amesema kuwa kuna haja ya wadau wa utalii pwani kubuni mikakati itakayosaidia kuboresha sekta hio ambayo kwa sasa imetajwa kusambaratika.

 Wakati uo huo ameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kushirikiana na wamiliki wa hoteli za watalii ndani ya mji huo ilikuimarisha zaidi utalii.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.