Upanuzi wa bandari ya Mombasa waathiri vibaya uvuvi

June 7, 2018

Huku serikali ikiendeleza upanuzi wa bandari ya Mombasa, wavuvi katika kaunti ya Mombasa wamejitokeza na kudai kwamba sekta ya uvuvi imeathirika kutokana na upanuzi huo.

Akiongea kwenye warsha iliyowaleta pamoja wavuvi pamoja na washikadau katika mamlaka ya bandari nchini KPA iliyoandaliwa na shirika la kijami la Mombasa Port Civil Society Organisation Platform, Mwenyekiti wa vitengo vinavyosimamia fukwe za bahari Mombasa, Kelly Konde amesema kuwa shughuli nyingi za bahari zimechangia upungufu wa samaki.

Konde ameweka bayana kwamba hatua ya wawekezaji kupewa nafasi kuweka kampuni zao mbalimbali kwenye fuo za bahari imesababisha madhara makubwa kwa wavuvi.

Kwa upande wake afisa katika kitengo cha sheria katika mamlaka ya bandari Bi Wamuyu Ikegu amesema kuwa mikakati ya kuihusisha jamii  hususan wavuvi inandelea ili kujadiliana nao kuhusu maeneo maalum waliyotengewa  kuendeleza shughuli zao za uvuvi.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.