Upotofu wa maadili wapelekea elimu kudorora Kinango

May 14, 2018

KAMISHANA WA KAUNTI YA KWALE KARUKU NGUMO

Picha/Maktaba

Kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo, ametaja upotofu wa maadili kuwa sababu kuu ya kudorora kwa viwango vya elimu katika eneo bunge la Kinango.

Akiongea katika shule ya msingi ya Mpirani huko Kinango, Karuku ametaja mimba na ndoa za mapema pamoja na kutowajibika kwa baadhi ya wazazi kuchangia matokeo duni katika shule nyingi Kwale.

Ngumo amewahimiza wazazi kuipa kipau mbele elimu ya watoto wao, ili wafaulu katika maisha yao ya baadaye.

Ngumo amewaagiza  wadau wa elimu pamoja na maafisa wa utawala katika eneo hilo kupanga mkutano wa dharura  kujadili  na kuibuka na suluhu kwa changamoto  hizo.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.