“Ushamba ndio Swagg,”asema Sultan Wa Pwani

May 11, 2018

Kwa siku nyingi msanii Sultan wa Pwani amaeonekana akiwa tofauti na wasanii wenzake katika mtindo wa mavazi.

Msanii huyo hukosa kuendana na mikombo au trends ya mavazi na badala yake huamua kuvalia jinsi anavyojihisi yeye mwenyewe binafsi.

Katika mahojiano maalum hivi leo amefichua kuwa hapendi kuendana na mkombo na siku zote yeye huvalia chochote.

“Huu ushamba ndio Swagg, binafsi sipendi kufuata mkumbo. Mimi ni mtu Classic kwa sababu mavazi yangu sio ya mkumbo bali kile ninachohisi kukivaa,”amesema msanii huyo.

Je unadhani kuwa wasanii wanafaa kuvaa kulingana na mkumbo?

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.