Ushirikiano wa wanabodaboda na polisi waleta mafanikio Kilifi

July 2, 2018

Wahudumu wa bodaboda katika eneo la Malindi kaunti ya Kilifi wamepongeza ushirikiano wao na maafisa wa usalama katika kufichua washukiwa wa mauaji ya wahudumu wa bodaboda na wizi wa pikipiki zao.

Kulingana na Nguwa Nzaro mmoja wa wahudumu wa pikipiki visa hivyo vimepungua kwa takriban asilimia 30.

Nzaro amehoji kuwa mauaji ya wahudumu wa bodaboda yamekuwa tatizo kwao kwa zaidi ya miaka saba ambapo wahudumu wengi wameuawa nyakati za usiku na pikipiki zao kuporwa huku washukiwa wakikosa kukabiliwa.

Kwa sasa wahudumu hao wameapa kuendeleza ushirikiano huu ili kuimarisha zaidi biashara zao.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.