Utata waibuka kati ya Kilele na Gavana Samboja

June 7, 2018

Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kaunti ya Taita-taveta Godwin Kilele  ametofautiana na msimamo wa gavana Granton Samboja  kuhusu ujenzi wa nyumba ya gavana ,naibu gavana na spika wa bunge.

Kilele amesema matamshi ya gavana Samboja kwamba fedha zinazotengewa ujenzi huu zielekezwe kwa sekta ya elimu, kufadhili karo za wanafunzi ni jambo ambalo halitawezekana.

Kilele amefichua kuwa katika bajeti ya mwaka 2018 -2019 shilingi millioni 134 zimetengewa ufadhili wa wanafunzi kimasomo.

Awali gavana Samboja alikataa kuidhinisha ujenzi wa makao hayo na kuagiza fedha hizo zielekezwe kwa elimu ili kiwango cha fedha kinachotengewa elimu kifikie shillingi millioni 250.

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.