Utumizi wa mihadarati wachangia kuongezeka kwa dhulma za kijinsia

June 25, 2018

Utumizi wa dawa za kulevya katika kaunti ya Kilifi umetajwa kuwa chanzo cha ongezeko la dhulma za kijinsia.

Kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la kupambana na dhulma za kijinsia la CREAW kaunti ya Kilifi, utumizi wa dawa za kulevya umechangia asilimia 44.6 ya visa vya dulma za kijinsia, huku ushawishi kutoka kwa marafiki ukichangia kwa asilimia 14.2.

Afisa wa mipango katika shirika hilo Isabella Mwangi ameongeza kuwa asilimia 22.9 ya visa vya dhulma za kijinsia hutokea kwa watoto.

Isabella amekashifu vikali kauli inayotumiwa na washukiwa kujitetea kuwa watoto huwaruhusu kushiriki nao tendo hilo huku akizidi kuhimiza ushirikiano wa jamii nzima kukomesha dhulma.

Taarifa na Marrieta Anzazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.