Vijana wahimizwa kujiajiri

June 2, 2018

mwinyi1

Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi amewataka vijana kushirikiana kikamilifu na viongozi wao kuhakikisha suala la ukosefu wa ajira miongoni mwao linakabiliwa.

Akiongea mjini Mombasa Mwinyi amesema kuwa vijana wanafaa kubuni miradi ya kibiashara wajikimu kimaisha na kujitenga na kasumba kwamba kuna uhaba wa ajira.

Mwinyi  aidha amedai kwamba vijana wamesalia bila   ajira kwa kutokuwa na mbinu mbadala za kujipatia kipato huku akisisitiza  kuwa  iwapo watashirikiana kikamilifu na viongozi wao  tatitizo hilo la ukosefu wa ajira litakabiliwa.

Mbunge huyo hata hivyo amewataka wazazi wa Mombasa kuwapa mwelekeo watoto wao kuhusu jinsi ya kujimudu kimaisha iliwajitenge na masuala ya uhalifu.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.