Vijana waombwa kuachana na matumizi ya mihadarati ili kukuza soka

July 9, 2018

Wito umetolewa kwa vijana kule Malindi kunti ya Kilfi kuachana na utumizi wa mihandarati sawia na dawa za kulevya na badala yake wajihusihe na michezo mbali ilikuona wanaendeleza vipaji vyao.

Haya ni kwa mjibu wa mchezaji wa timu ya kitaifa Harambee stars ambaye pia anaichezea klabu ya Tottenham Hotspurs nchini Uingereza Victor Wanyama ambaye amewataka vijana ambao wanavipaji vya kucheza mpira kuzingatia maadili mema sawia na kuepuka dawa za kulevya .

Akizungumza wakati alipoitembela timu ya Malindi United Wanyama aliyekuwa ameandamana na nduye MacDonald Mariga amesema uraibu wa mihadariti miongoni mwa wachezaji ndio chanzo cha kushusha hadhi ya mchezaji sambamba na timu yake.

Aidha Mariga ambaye anachezea timu ya Real Oviedo iliyoko nchini Uhispania amesema soka la humu nchini litaimarika pindu tu vijana watakapo susia utumizi wa dawa za kulevya ambao kwa sasa asilimia kubwa ya vijana walioko nyanjani hujiingiza kwa urahisi.

Hata hivyo familia hiyo ya Wanyama imetoa shilingi 50,000 na mipira 5 kwa timu ya Malindi United ili kuzidi kuinua vipaji miongoni mwa wachezaji.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.