Vijana washauriwa kujitenga na vurugu

November 28, 2017

Mwanaharakati wa masuala ya Uiano na utangamano katika kaunti ya Kilifi Athman Said amewashauri vijana kutokubali kutumiwa vibaya na viongozi wenye nia potofu ili kuzua vurugu wakati ya hafla ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta.

Akizungumza na Wanahabari mjini Malindi, Said amesema kuwa kuna haja ya wafuasi kutoka pande zote mbili kukubali uamuzi uliotolewa na mahakama ya upeo ili taifa lisalie na amani.

Said amewaomba wananchi kudumisha amani kabla, wakati na hata baada ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Kenyatta, akisema kuwa vurugu za kila mara hudidimiza uchumi wa taifa.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.