Vilabu vya michezo kupata ufadhili Kwale

November 16, 2017

Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Usimamizi wa Talanta wa kaunti ya Kwale, Ramadhan Bungale, amesema kuwa wizara yake itawapa vijana nafasi ya kukuza talanta zao katika fani mbalimbali za michezo.

Akizungumza na meza yetu ya michezo kwenye kikao maalum, Bungale amesema kuwa wapo katika harakati ya kuvitafutia vilabu vya michezo mbalimbali ufadhili ili viweze kuendeleza talanta zao.

“Tayari tumezungumza na wafadhili kadhaa ambao watakuwa wanazuru kaunti ya Kwale ili kuthathmini talanta za vijana wetu wale watakaofanikiwa watapawa ufadhili,” amesema Bungale.

Kulingana na waziri huyo vijana wa kaunti ya Kwale wanaweza kujibunia nafasi za kazi iwapo talanta zao zitatiliwa manani.

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.