Viongozi wa kidini wamtaka Raila kusitisha azma ya kuapishwa

January 10, 2018

Viongozi wa kidini wa Malindi kaunti ya Kilifi sasa wanamtaka Kinara wa Muungano wa NASA Raila Odinga kusitisha azma yake ya kutaka kuapishwa na badala yake kushiriki mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta.

Akizungumza na Wanahabari mjini Malindi, Askofu wa Kanisa la Kiangalikani jimbo la Malindi Lawrence Dena amesema kuwa hatua ya Odinga huenda ikaleta mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wananchi.

Askofu Dena amesema kuwa Odinga anastahili kusitisha mara moja mipango yake na kuhakikisha ana waunganisha wakenya wote kwa kuzingatia kanuni na Katiba ya nchi.

Wakati uo huo amewashauri wakenya kuhubiri amani, umoja na utangamano sawia na kueka kando tofauti zao kisiasa, kikabila na kidini.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.