VIONGOZI WA KIDINI WASHAURIWA KUKEMEA UKIUKAJI WA HAKI ZA KIBINADAMU

October 26, 2018

Mkurugenzi mkuu wa shirika linalopigania maswala ya amani na usalama Pwani Kenya Community Support Centre Bi. Phyllis Muema amesema kuwa dhulma na ukiukaji wa haki za kibinadamu Pwani utakomeshwa iwapo viongozi wa kidini watakemea tabia hii.

Bi. Muema amedai kuwa viongozi wa kidini wamesalia kimya licha ya kuwa na ushawishi na mchango mkubwa katika kuibadili hali hii.

Akizungumza katika afisi za shirika hilo Kisimani kaunti ya Mombasa, Bi. Muema amewataka viongozi wa kidini kuwaelezea waumini wao jukumu la maafisa wa usalama, jamii na mashirika ya utetezi wa haki, ili kuhimiza uiano na kukomesha dhuluma na mauaji ya kiholela pwani.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.