Viongozi wa kisiasa Mjini Mombasa wapuuza ziara ya Netanyahu.

July 21, 2016

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir pamoja na Senet wa Kaunti ya Mombasa Omar Hassan. Wawili hao wameshirikiana na Viongozi wa dini ya Kiislamu kukashfu ushirikiano kati ya Kenya na taifa la Israel.

Viongozi wa kisiasa na wale wa dini ya Kiislamu Mjini Mombasa wamepuuzilia mbali ziara ya siku tatu ya hivi majuzi ya Waziri mkuu wa nchi ya Israel Benjamin Netanyahu.

Wakiongozwa na Seneta wa Kaunti ya Mombasa Omar Hassan, Viongozi hao wamesema kwamba mikataba iliyotiwa saini ya kiusalama na maendeleo kati ya Netanyahu na Rais Uhuru Kenyatta inalenga kuliweka taifa hili katika athari zaidi ya uvamizi wa kigaidi hasa ikizingatiwa kwamba Israel inalengwa sana na magaidi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ameunga mkono kikamilifu kauli ya Omar na kusisitiza kwamba Israel imekuwa mstari wa mbele katika kuwakandamiza Waislamu duniani hivyo basi Kenya haifai kushirikiana na taifa hili kivyovyote vile.

Akitoa kauli sawa na hiyo, Kadhi mkuu wa zamani nchini Sheikh Ahmed Mohammed Kassim amesema kwamba hatua hiyo ya Kenya kuweka mikataba ya kiusalama na maendeleo kati yake na Israel huenda ikaiweka Kenya machoni pa magaidi hali itakayowatia hofu zaidi Wakenya.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.