Viongozi wa kisiasa wahimizwa kuiunganisha jamii

January 29, 2019

Mwenyekiti wa makundi mbalimbali ya walemavu katika kaunti ya Mombasa Bi Hamisa Maalim Zajah amewataka viongozi wa kisiasa humu nchini kuhakikisha wako katika mstari wa mbele na kuzileta jamii pamoja ili taifa hili liwe la amani.

Akizungumza kule mjini Mombasa, Bi Zajah amesema iwapo kiongozi ameshindwa kuwajumuisha wananchi wake pamoja ama kushuhudiwa mgogoro ndani ya vyama basi kiongozi kama huyo hafai kuwaonga wananchi.

Bi Zajah amesema kuwepo kwa maridhiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga maarufu kama Handshake ilikuwa ni kuwaleta wakenya pamoja lakini kinachoshuhudiwa kwa sasa ni migawanyiko sio kuwa na msingi wowote.

Hata hivyo amesema taifa la Kenya lingali bado linahitaji maendeleo na umarishaji uchumi hivyo basi akamshauri kiongozi wa nchi kushikamana vyema na viongozi mbalimabali ili kufanikisha miradi ya maendeleo.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.