Viongozi wahimizwa kuwa na uiano

February 10, 2019

Uiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga unapaswa kutiririka mashinani ili viongozi wote wabadili mtazamo wao wa kisiasa na kulishughulikia vilivyo swala la maendeleo kwa wananchi.

Kiongozi wa vijana wa eneo la Tononoka mjini Mombasa Abdulrahman Abdulhamid amesema kwamba uiano huo kamwe haupaswi kutazamwa kama jambo dogo la ngazi za juu na badala yake kama muelekeo wa taifa hasa katika swala la uongozi, maendeleo na demokrasia.

Akizungumza Mjini Mombasa , Abdulhamid amesema kwamba ni sharti viongozi wa kisiasa wawache migawanyiko yao ya kisiasa na kuwagawanya wakaazi hasa katika eneo la Pwani na badala yake walishughulikie barabara swala la maendeleo pasipo na ubaguzi.

Mwanaharakati huyo wa Vijana hata hivyo amewataka Viongozi kuwajibika na wala sio kupiga siasa zisizokuwa na msaada wowote kwa Wakaazi wa Kaunti hiyo ya Mombasa.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.