Viongozi wapwani washambuliwa kwa kukosa kutatua utata wa ardhi

April 28, 2018

Shirika la ‘Residents Land Protection Organization of Kenya’ limewashambulia viongozi wa eneo la Pwani kwa kushindwa kufanya mkao wa pamoja na kulijadili kuhusu kubuni mbinu za kuhakikisha mkaazi wa Pwani ana miliki ardhi yake.

Mwenyekiti wa Shirika hilo, Dewelly Nyambu amesema licha ya viongozi hao kutoa ahadi za mara kwa mara kuhusu kuyatatua maswala ya ardhi Pwani, hakuna hatua zozote ambazo zimeafikiwa.

Kulingana na Nyambu, eneo la Pwani limeshuhudia msururu wa visa vya unyakuzi wa ardhi na wakaazi kufurushwa katika ardhi zao, huku Serikali ikionekana kushirikiana na mabwenyenye.

Nyambu anapendekeza viongozi hao kusimama imara na mpwani na kushirikina na wakereketwa wa maswala ya ardhi ili kulikabili tatizo hilo na kuhakikisha pwani hafurushwi kwenye ardhi yake.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.