VIONGOZI WASHAURIWA KUIBUKA NA SULUHU KWA UHABA WA CHAKULA

December 4, 2017

Mwakilishi wa wadi ya Gongoni kaunti ndogo ya Magarini Albert Kiraga, amewashauri viongozi katika eneo hilo kuibuka na mikakati kuhakikisha kwamba tatizo la uhaba wa chakula kwa wakazi katika kaunti hiyo linapata suluhu la kudumu.

Kulingana na Kiraga takriban asilimia 54 ya wakazi wa Kilifi wameathirika na baa la njaa.

Hata hivyo, Kiraga ametilia mkazo suala la wakazi kutumia mbinu zilizoboreshwa za kilimo na kupanda mimea mbali mbali wakati wa mvua ili kuimarisha kiwango cha chakula kinachozalishwa.

Mwakilishi huyo wa wadi ya Gongoni ametaja maeneo ya Ganze, Magarini na Kaloleni kuwa maeneo yalioathirika zaidi na uhaba wa chakula anaosema umechangia ongezeko la kiwango cha umaskini.

Taarifa na Esther Mwagandi

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.