VIONGOZI WATOFAUTIANA KUHUSU MARUFUKU YA SERIKALI.

June 6, 2018

Vuta nikuvute inashuhudiwa baina ya viongozi eneo la Magarini na maafisa wa idara ya misitu kuhusu marufuku ya ukataji miti na uchomaji makaa iliyowekwa na serikali.

Hii imeshuduhiwa baada ya mwakilishi wa wadi ya Marafa katika bunge la kaunti ya Kilifi Renson Kambi kushikilia msimamo kwamba baadhi ya maeneo katika ardhi ya ranchi ya Dakatcha Woodland ni makazi ya  wananchi ambayo idara ya misitu haifai kuingilia.

Kambi aidha anadai kuwa marufuku dhidi ya uchomaji makaa imewaacha wakazi wengi bila ajira akihimiza makaa yote ambayo tayari yalikuwa yamechomwa kutoharibiwa na badala yake wakaazi waruhusiwe kuyauza.

Hata hivyo afisa mkuu wa idara ya misitu eneo la Malindi na Magarini Harrison Afuata amepuzilia mbali pendekezo la kuendeleza biashara ya makaa na badala yake akasisitiza kuwa makaa yote yatakayonaswa yataharibiwa kutii amri ya serikali.

Taarifa na Charo Banda

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.