Viwavi jeshi vyazua wasiwasi Taita Taveta

November 27, 2017

Wakulima katika kaunti ya Taita Taveta wanahofia kwamba huenda kaunti hiyo ikakumbwa na uhaba wa chakula kufuatia uharibifu wa mimea unaosababishwa na viwavi jeshi.

Kwa mujibu wa Rashid Seif, mmoja wa wakulima hao uharibifu wa mimea yao utawasababishia njaa kwa familia zao kwani chakula cha msaada kinachotolewa na serikali ya kitaifa hakitoshi.

Afisa mkuu wa kilimo kaunti ya Taita Taveta Evans Mbinga amethibitisha kwamba serikali ya kaunti kupitia wizara ya kilimo inasambaza madawa kwa wakulima kukabiliana na viwavi jeshi hao wanaosemekana kuingia humu nchini kutoka nchini Rwanda.

Hata hivyo juhudi hizo zinakabiliwa na changamoto kubwa huku maafisa wa kilimo nyanjani wakilalamikia hali ya wakulima kutofuata maagizo ya jinsi ya kutumia dawa ya kudhibiti mdudu huyo.

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.