Wabunge waasi wa ODM watakiwa kujiuzulu

January 7, 2019

Viongozi mbalimbali wa chama cha ODM.

Viongozi mbalimbali wa chama cha ODM.

Wanachama wa Chama cha ODM katika eneo bunge la Msambweni chini ya vuguvugu la Ngumu Tupu Handshake, wameshinikiza wabunge waasi wa chama hicho kujiuzulu kutoka chama hcha ODM.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Vuguvugu hilo, Chitembe Hassan, wanachama hao wanamtaka Mbunge wa Msambweni Suleiman Dori na mwenzake wa Malindi Aisha Jumwa kuondolewa katika chama hicho kufuatia hatua yao ya kukiasi chama cha ODM.

Chitembe amewakosoa vikali wabunge hao wawili kwa kile alichokitaja kama ukosefu wa heshima kwa Kinara wa chama hicho Raila Odinga pamoja na Naibu wake Ali Hassan Joho huku akisisitiza kuwa wawili hao wanafaa kufukuzwa kwa chama.

Wakati uo huo ameshinikiza kufutiliwa mbali kwa baadhi ya nyadhfa za uongozi kama vile wajumbe wa Wadi, maseneta pamoja na Wawakilishi wa Kike, akisema nyadhfa hizo zinawagharimu wakenya.

Taarifa na Salim Mwakazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.