Wadau wa sekta ya elimu Malindi wataka uchunguzi wa kina kufanyika kuhusu mgomo wa wanafunzi

July 12, 2018

Wadau wa sekta ya Elimu katika kaunti ya Kilifi, sasa wanaitaka serikali kupitia wizara ya elimu kuchunguza kwa kina chanzo cha migomo ya wanafunzi inayoshuhudiwa katika shule mbali mbali nchini.
Mkurugenzi wa shule ya kibinafsi ya Malindi Progressive Rashid Odhiambo amesema huenda migomo ya mara kwa mara ya wanafunzi inatokana na msukumo kutoka kwa baadhi ya wafanyikazi wa shule wanakosomea wanafunzi hao.
Mdau huyo wa elimu amehimiza usimamizi wa shule kufuatilia kwa karibu mienendo ya wafanyikazi wake akidai kuwa wanafunzi hawawezi kutekeleza uharibifu pasi na wafanyikazi wa shule kufahamu.

Aidha Odhiambo amedai  kuwa uhuru wa wanafunzi pia umechangia pakubwa utovu wa nidhamu shuleni hasa katika shule za umma akihimiza serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wote wa visa hivyo.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.