Wadi ya Garashi yapata shilingi milioni 2.5 kutoka kwa serikali ya kaunti

January 10, 2018

Mwakilishi wa wadi ya Garashi huko Magarini kaunti ya Kilifi Peter Ziro amesema kwa amepokea jumla ya shilingi milioni 2.5 katika awamu ya kwanza kutoka kwa Serikali ya kaunti hiyo ili kufadhili wanafunzi waliofanya vyema.

Ziro amesema kuwa fedha hizo zinawalenga hasa wanafunzi werevu pamoja wale wanaotoka katika familia zisizojiweza huku akisema kuwa tayari kamati inayohusika na masuala hayo imeanza kuzikagua fomu ambazo wanafunzi walijaza.

Ameongeza kuwa serikali ya kaunti hiyo pia inalenga kutoa kitita chengine hivi karibuni cha shilingi milioni 2.5 katika awamu ya pili na awamu ya tatu akitarajiwa kupokea shilingi milioni tano ili kukamilisha mradi wa kufadhili wanafunzi.

Hata hivyo, amewashauri wazazi wa eneo hilo kuhakikisha wanawajibikia vyema elimu ya watoto wao badala ya kuweka mtazamo kwa viongozi wa kisiasa.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.