Waekezaji wahimizwa kuzingatia sheria za mazingira

November 30, 2017

Katibu mkuu wa wizara ya Mazingira na Mali Asili nchini Dkt Magaret Mwakima amewatolea mwito waekezaji kote nchini kuzingatia Sheria za uekezaji ili kujenga uwiano bora Kati yao na jamii.

Kulingana na Dkt Mwakima waekezaji wengi hawafuati sheria wanapoendeleza shughuli za uekezaji hasa zinazohusiana na athari za kimazingira kabla ya kutekeleza miradi yao.

Dkt Mwakima aliyekuwa akizungumza katika warsha ya kujadili maswala ya raslimali nchini ililofanyika katika hoteli moja huko Diani kaunti ya Kwale amewataka wadau katika sekta ya mazingira na mali asili kushirikiana na kuhakikisha mazingira na  mali asili zinatunzwa vyema.

Kwa upande wake Jared Bosire kutoka Shirika linalojishuhulisha na masuala ya uhifadhi wa mazingira la WWF amesema kwamba shirika hilo litatoa muongozo bora na kuibuka na sera zitakazotumika kulinda na kuboresha raslimali nchini.

Taarifa na Mwanakombo Juma.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.