Wafanya kazi wa mashirika ya kijamii waishi kwa hofu Kenya

February 11, 2019

Mashirika ya kijamii humu nchini yamedai kuishi kwa hofu kutoka na kuongezeka kwa visa vya mauaji na kupotea kwa watu katika hali tatanishi.

Kulingana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Haki Afrika Hussein Khalid, visa vya vitisho kwa wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu vimekithiri mno na kuna haja ya kukomeshwa mara moja.

Akizungumza na Wanahabari, Khalid amesema ni wazi kuwa vitengo vya usalama humu nchini vimezembea kuwjibikia majukumu yao ya kuimarisha usalama na kusababisha visa vya watu kutetea kiholela kuongezeka.

Kwa upande wake Naibu mkurugenzi wa Shirika hilo Salma Hamed amesema kama Shirika hawatasitisha juhudi zao za kupambana na visa vya dhulma na unyanyasaji kwa jamii.

Kauli zao zimejiri baaada ya Mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu wa Shirika la ‘Dandora Social Justice Center’, Caroline Mwatha kupotea katika hali tatanishi.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.