Wajawazito wataabika baada ya barabara kukatika Chanagande

May 10, 2018

Akina mama wajawazito na wanaotafuta huduma za kliniki kwa watoto wao katika eneo la Kaloleni kaunti ya Kilifi wamelalamikia kukumbwa na changamoto za usafiri baada ya barabara ya Chanagande kukatika kufuatia mafuriko.

Akiongea  na meza ya muliko katika eneo la Chalani Mapenzi  Charo aliye mmoja wa akina mama hao amelalamikia ongezeko la nauli wanayotozwa na wahudumu wa pikipiki.

Akina mama wengi wajawazito wamelazimika kujifungulia majumbani kutokana na hali mbaya ya barabara hiyo.

Akina mama hao sasa wanatoa mwito kwa viongozi  katika eneo hilo kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo ili shughuli za usafiri ziregelee hali yake ya kawaida.

Taarifa na Mercy Tumaini.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.