Wajumbe 400 kutoka Kwale wahudhuria kuapishwa kwa Rais

November 29, 2017

Zaidi ya wajumbe 400 kutoka kaunti ya Kwale walihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani jijini Nairobi.

Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya aliongoza ujumbe huo kuonyesha uungaji mkono kwa Rais na naibu wake na chama cha Jubilee kwa ujumla.

Kaunti  ya Kwale ni kati ya kaunti mbili katika ukanda wa Pwani ambazo zilichagua magavana waliosimama na chama cha Jubilee kwenye uchaguzi wa Agosti Nane.

Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliapishwa siku ya Jumanne katika uwanja wa Kasarani.

Taarifa na Radio Kaya.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.