Wajumbe wa ODM wataka waasi wa chama kuchukuliwa hatua

July 12, 2018

Wajumbe kutoka bunge la kaunti ya Kilifi wamekitaka chama cha ODM kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi wote waliokiasia chama hicho.

Wakihutubia waandishi wa habari nje ya makao makuu ya bunge hilo, wajumbe hao wakiongozwa na mwakiIishi wa wadi ya Kakuyuni Nickson Mramba, wamesema viongozi wa chama hicho wanaoendelea kumpigia debe naibu wa rais William Ruto katika azma yake ya kuwania urais mwaka wa 2022 wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa kukiuka sheria za chama.

Aidha wametoa mwito kwa viongozi walio kiasi chama hicho kujitokeza wazi na kuelezea mwelekeo wao kisiasa badala ya kuwahadaa wananchi hao kwa kisingizio kuwa wanashirikiana na viongozi wa Jubilee kupata miradi ya maendeleo.

Kwa kauli moja wajumbe hao wamemtaka katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna na kinara wake Raila Odinga kuwatimua mara moja waasi wote wa chama hicho.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.