Wakaazi wa Freretown wataka mradi wa Methadone uondolewe

June 22, 2018

Mradi wa kliniki ya kuwatibu waraibu wa dawa za kulevya wa “Methadone” ulioko Freretown huko Nyali umepatwa na pigo.

Mradi huo unaotekelezwa na Serikali ya Kaunti ya Mombasa kwa ushirikiano na Shirika la kupambana na dawa za kulevya nchini NACADA, lile la ‘Reachout Centre Trust’ na Afisi ya umoja wa mataifa ya kupambana na dawa za kulevya ‘United Nation Office Against Drugs and Crime-UNODC, unasemekana kuwa unaathari mbaya  kwa kizazi kichanga katika eneo hilo.

Akikiri kuwepo kwa utata huo, Afisa mkuu wa Shirika la kupambana na dawa za kulevya NACADA Kanda ya Pwani George Karisa ameahidi kujailiwa kwa suala hilo na wadau wanaotekeleza mradi.

Karisa amesema kwamba kliniki hiyo inayowahudumia zaidi ya waraibu 800 ambao wameasi uraibu na kupewa tiba hiyo kila siku ina umuhimu mkubwa kwa waraibu hao.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.