Wakenya waongoza East Africa Classic Safari Rally

November 30, 2017

Mashindano ya East Africa Classic Safari Rally yanaingia siku yake ya 8 hivi leo huku Mkenya Baldev Sign Chager ndiye akiongoza kwa muda wa jumla wa 377.34 akiendesha gari aina ya Porsche 911.

Wapili ni Richard Jackson anayesaidiana na Ryan Champion wakiendesha gari aina ya Porsche 911 wakiwa na muda wa 379.13.

Nafasi ya tatu inashikiliwa na mkenya Carl Tundo akisaidiana na Tim Jessop wakiendesha gari aiana ya Triumph TR7 wakiwa na muda wa 385.32.

Wanoshikilia nafasi ya nne ni  raia wa Afrika kusini Geoff Bell akisaidiana na Tim Challen wakiendesha gari aina ya Datsun 260z wakiwa na muda wa 399.48 na watano ni Raaj Bharji akisaidiana na Rajay Sehmi kutoka kenya wakiendesha gari aina ya Porsche 911 wapo na muda wa 408.06.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.