Wakimbizi waliorudishwa makwao wateseka – Amnesty International

December 18, 2017

Shirika la Kimataifa la utetezi wa haki za kibinadamu la Amnesty International limesema kurudishwa kwa wakimbizi nchini Somalia kumechangia mateso na hali ngumu ya kimaisha kwa wakimbizi hao.

Kulingana na Afisa anayesimamia haki za wakimbizi katika Shirika hilo Mohammed Adan, wakimbizi waliorudishwa nchini Somali kutoka kwa kambi ya Dadaab mwaka uliopita wanaishi katika hali ya taabu.

Mohammed amesema kwamba wakimbizi hao wameshindwa kutambua makazi yao asilia kwani wengi wao walizaliwa kambini huku akisema kuwa serikali ya Kenya ingeangazia maslahi yao hasa baada ya shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia maswala ya wakimbizi la UNHCR kuingilia kati.

Hata hivyo Shirika hilo linashikilia kwamba licha ya mahakama kuzima juhudi za Serikali za kuifunga kambi hiyo ya wakimbizi, mikakati hiyo imekuwa ikiendelezwa kisiri na wakimbizi wengi kushurutishwa kurudi nchini kwao.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.