Wakulima walalamikia uharibifu wa Ndovu

November 30, 2017

Wakulima katika vijiji vya Makwasinyi, Bughuta na Kasighau huko Voi kaunti ya Taita Taveta wanakadiria hasara kubwa baada ya kundi la ndovu wanaodaiwa kutoroka kutoka mbuga za Tsavo kuvamia mashamba yao.

Wakulima hao wakiongozwa na Douglas Mwamburi wanasema kuwa juhudi za Shirika la huduma kwa wanyamapori (KWS) kukabiliana na ndovu hao hazijafauli kwa siku nne sasa.

Mwamburi ameitaka idara hiyo kutuma maafisa zaidi ili kusaidia katika operesheni ya kuwarudisha ndovu hao mbugani.

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.