Wakulima washauriwa kugeukia kilimo biashara

November 29, 2017

Afisa wa Kilimo katika eneo la Magarini kaunti ya Kilifi Lilian Kirombo amewataka wakulima kuzingatia Kilimo biashara badala ya kilimo cha kuzalisha chakula cha nyumbani pekee.

Lilian amesema kuwa wakulima wanafaa kuzingatia kilimo cha mimeo mingine kando na mahindi hatua ambayo itawawezesha wakulima kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga hasa wakati wa mvua chache.

Akizungumza katika eneo la Sosoni/Marafa huko Magarini, Lilian amewahimiza wakulima kuzingatia kilimo cha kisasa na kutumia mbegu ambazo hustahimili kiangazi.

Kwa upande wake mkulima maarufu ambaye pia ni Mwakilishi wa Wadi katika eneo hilo Renson Kambi amepuzilia mbali dhana kuwa ukulima ni shughuli ya wazee na akawataka vijana nao kujihusisha na kilimo biashara.

Taarifa na  Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.