Walio jenga kwenye ardhi za umma waonywa

November 19, 2018

Katibu katika Idara ya huduma za umma nchini Paul Mwangi amewaonya vikali wenye tabia ya kujenga mijengo yao kwenye ardhi za umma hususan katika fuo za bahari kuwa watakabiliwa kisheria.

Mwangi amesema tayari idara hiyo inapania kuzuru mashinani na kuzivunja nyumba zilizojengwa kwenye ardhi za umma bila idhini ya serikali, akisema hatua hiyo ni unyakuzi wa ardhi za umma.

Amesema pia watabomoa nyumba ambazo zimejengwa kwenye mitaro ya kupitisha maji taka kwani ni hatari kwa afya ya wananchi.

Wakati uo huo amewataka wakenya kuheshimu sheria za ujenzi humu nchini sawia na kufuata vigezo vinavyohitajika wanapotaka kujenga mijengo yao.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.