Wanafunzi 100 wapata ufadhili Taita Taveta

January 10, 2019

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja.

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja.

Jumla ya wanafunzi 100 kutoka kaunti ya Taita Taveta waliopata alama 300 na zaidi katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE mwaka jana, wamepata ufadhili wa masomo ya shule za upili kutoka kwa serikali ya kaunti hiyo.

Akiongea alipoongoza zoezi hilo, Gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja amesema tayari wameiandikia barua hazina kuu ya fedha nchini, kusambaza fedha za kutosha kwa kaunti hiyo.

Samboja ametoa wito kwa wadau wote wa sekta ya elimu kushirikiana ili kuviboresha viwango vya elimu katika kaunti hiyo huku akiwataka wazazi kuwajibikia majukumu yao ya ulezi.

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.