Wanafunzi 130 wapata ufadhili Ganda

January 13, 2018

Takriban wanafunzi 130 wanaotoka familia zisizojiweza kutoka wadi ya Ganda kaunti ya Kilifi wamenufaika na usaidizi wa karo ya kima cha shilingi milioni mbili unusu kutoka kwa hazina ya basari ya wadi hiyo.

Akiongea katika eneo la Kijiwe Tanga wakati wa kupeana hundi ya pesa hizo Mwakilishi wa Wadi ya Ganda, Abdulrahman Omar amesema kuwa kufikia sasa kuna zaidi ya wanafunzi 700 katika wadi hiyo wanaohitaji usaidizi wa karo ili waendelee na masomo yao.

Omar amehoji kuwa mgao wa fedha unaotengwa wadi hiyo wa shilingi milioni kumi kwa kila wadi hautoshi ikilinganishwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaohitaji usaidizi wa karo.

Kwa upande wake Susan Kasichana  mmoja wa wazazi walionufaika na usaidizi huo  amesema kuwa imekua changamoto  kwa wanafunzi katika eneo hilo kupata elimu kutokana na viwango vya juu vya umasikini kwa familia za eneo hilo.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.