Wanafunzi elfu 2 wanufaika na Basari Jomvu

May 6, 2018

Zaidi ya wanafunzi elfu 2 wa shule za upili kutoka eneo bunge la Jomvu, Mombasa wamenufaika na fedha za basari.

Akiongea wakati wa kupeana hundi ya basari ya zaidi shilingi milioni 11, Badi amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha sekta ya elimu sawa na kuwaepusha watoto kujihusisha na masuala ya mihadarati na uhalifu.

 Badi aidha amewataka wazazi katika kaunti ya Mombasa kwa jumla kushirikiana kikamilifu na viongozi wao kuhakikisha kwamba viwango vya elimu eneo hilo vinaimarika.

Badi amefichua kwamba kutotiliwa mkazo kwa Swala la elimu kumechangia pakubwa kudorora kwa viwango vya elimu katika maeneo ya mashinani.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.