Wanafunzi kutoka shule 10 kukumbwa na janga la Njaa Kilifi

May 29, 2018

Huenda wanafunzi katika takriban shule kumi za msingi eneo la Lango Baya kaunti ya Kilifi wakakumbwa na uhaba wa chakula baada ya mradi mkubwa wa kilimo waliotegemea kupata lishe kusambaratika.

Mradi huo wa takriban shilingi milioni nne ambao wamekuwa wakitegemea kuzalisha vyakula mbali mbali umesambaratika baada ya takriban ekari 35 za mahindi kusombwa na maji ya mafuriko.

Kulingana na mshirikishi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Karibun Onlus linalofadhili mradi huo, Jackson Ole Kanai chakula kilichosalia kwa sasa kitatosheleza wanafunzi hao kwa kipindi cha miezi miwili pekee.

“Italazimika tusimamishe mradi wetu wa feeding program. Kwa sasa tumepunguza posho katika baadhi ya shule na tutakuwa tunawalisha siku tatu kwa wiki lakini tukimaliza vile vyakula tuko navyo kwa gala kwa sasa hatuna mwelekeo wa vile tutafanya,”amesema Kanai.

Mshirikishi huyo vilevile ameitaka serikali ya kaunti ya Kilifi pamoja na serikali kuu kuingilia kati na kuendeleza mpango huo wa lishe.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.