Wanafunzi waliofanya vyema Jilore wahakikishiwa ufadhili

January 12, 2018

Mwakilishi wa wadi ya Jilore kaunti ya Kilifi Daniel Chai Chiriba amewahakikishia wanafunzi katika eneo hilo waliofanya vyema kwenye mitihani ya kitaifa kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi itawapa ufadhili wa masomo.

Kulingana na Chiriba, ukaguzi wa wanafunzi waliojaza fomu kuomba msaada wa kimasomo unaendelea.

Kiongozi huyo amewahimiza viongozi wengine kutoka kaunti hiyo kulipatia kipau mbele suala la Elimu akiitaja kama msingi wa maendeleo.
Vile vile amewahimiza wanafunzi watakaonufaika na msaada huo kutia bidii zaidi masoni ili kutimiza malengo yao katika siku za usoni.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.