Wanaharakati wa haki za kibinadamu waishinikiza kaunti ya Mombasa kudhibiti mkurupuko wa Kipindupindu

November 25, 2017

Wanaharakati wa maswala ya kijinsia na haki za watoto kaunti ya Mombasa wameitaka Serikali ya Kaunti hiyo kuwekeza katika kuukabili mkurupuko wa ugonjwa wa Kipindupindu  kabla ya maafa zaidi kushuhudiwa.

wakiongozwa na afisa wa Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini Haki Afrika Bi Salma Hemed wanaharakati hao  wamesema kwamba ni sharti Kaunti hiyo ifanye juhudi zaidi katika kuudhibiti ugonjwa huo.

 Kwa upande wake Waziri wa afya Kaunti ya Mombasa Bi Hazel Koitaba amesema kuwa maafisa wa serikali ya Kaunti hiyo wanazuru mashinani ili kufunga vibanda vya chakula vilivyo katika mazingira machafu.

Tayari watu wawili wameripotiwa kufariki kufuatia ugonjwa huo, huku visa 25 vya ugonjwa huo vikiripotiwa katika mitaa ya mabanda ya Kalahari, Bangladesh, Morotto pamoja na maeneo ya Mishomoroni eneo la Kisauni.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.