WANAHARAKATI WAANDAMANA KUPINGA DHULMA ZA KIJINSIA

June 6, 2018

Wanaharakati wa kupambana na dhulma za kijinsia Watamu kaunti ya Kilifi wameandamana kupinga kukithiri kwa visa vya dhulma za kijinsia hasa kwa wanafunzi.

Wanaharakati kutoka shirika la Sauti Ya Wanawake huko Watamu wameandamana hadi ofisi ya chifu huku wakiwa wamebeba mabango wakikemea visa hivyo.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Roselyne Naabala wanaharakati hao wameapa kupiga vita dhulma hizo huku wakiitaka serikali kuhakikisha wanafunzi hasa wa kike wako salama wakiwa shuleni.

Kauli yake imeungwa mkono na kiongozi wa walemavu huko Watamu Linet Mkutano, aliyesema kuna haja ya mahakama kuweka sheria na  adhabu kali ikiwemo kifungo cha maisha kwa yeyote atakayepatikana kutekeleza unyama huo.

Taarifa na Charo Banda

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.