Wanaoendeleza biashara haramu ya Shisha waonywa

January 31, 2019

Huku wizara ya Afya nchini ikiendeleza juhudi za kuhamasisha wakenya kuhusu athari za matumizi ya Shisha, imebainaka kuwa kuna baadhi ya sehemu nchini zingali zinaendeleza biashara hiyo haramu.

Afisa katika wizara hiyo Pauline Ngari ametaja hatua hiyo kama imechangia marufuku hiyo kutofaulu na kupelekea wakenya wengi kuendelea kuathirika na utumizi wa uvutaji wa Shisha.

Aidha amewaonya vikali wafanyibiashara wanaoendeleza biashara hiyo kisiri, akisema watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake Afisa mkuu wa Shirika la NACADA kanda ya Pwani George Karisa amesema kama Shirika wanapania kuanzisha hamasa maalum shuleni kuhusiana athari ya Shisha.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.