Wanaojihusisha kimapenzi na watotowa shule waonywa Bamba

February 5, 2019

Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire ameonya vijana na wanawake wanaojiingiza kwenye uhusianao wa kimapenzi na watoto wa shule ya Jila eneo la Bamba kaunti ya Kilifi kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

Teddy amesema kuwa visa kadhaa vimeripotiwa vya akina mama na vijana kuwaeka kinyumba wanafunzi wa shule hio kwa kisingizo kwamba wanawapa hifadhi.

Mbunge huyo wa Ganze amesema kuwa ukosefu wa mabweni katika shule hiyo na mahitaji mengine muhimu ya wanafunzi hasa wakike imechangia pakubwa kushuhudiwa kwa visa hivyo.

Taarifa na Marieta   Anzazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.